[...] "Nina pendekezo."Likaegemea mbele kama rafiki yangu April anavyofanya anapotaka kusema siri,ijapokuwa hakuna siri yake yoyote iliyo nzuri. Ama kwa kweli siri. " Kama hutamwambia yeyote niko hapa, ninaweza tengeneza macho yako."
"Toka nje ya mji!"
Likapepesa mara kadhaa. "Hilo ndilo ninalojaribu kufanya."
"Mbona sivyo?"
"Vema,hakuna mwingine yeyote aliyeweza kutengeneza macho yangu pasipo na kutumia miwani."
"Nina uwezo fulani. Utaona,alimradi..."
"...sitamwambia yeyote kukuhusu?"
"Huo ndiyo moyo wake,hicho ndicho kiini."
"Nitajuaje kwamba hutanipofusha? Unaweza kuwa mmoja wa wale wanasoko wa simu wanaotoa ahadi ila wanadanganya."
Likaanza kupevuka na kupungua tena. "Siwezi fanya jambo kama hilo kwa kiumbe ambaye hajanidhuru."
"Kumaanisha kuwa iwapo ningekudhuru,ungenipofusha?"
"Hilo ni kwa misingi ya iwapo unahitaji kujua."
"Na iwapo utatengeneza macho yangu na nisimwambie yeyote,utaondoka kwenye mashamba yetu?"
"Hicho ndicho kiini chake!" [...]