[...] "Nina pendekezo." Kikainama mbele kama rafiki yangu April anafanya anapotaka kusema siri, ingawa hakuna siri zake nzuri. Au hata siri za kweli. "Usipoambia yeyote kuhusu mimi kuwa hapa, Naweza kuponya macho yako."
"Ondoka mjini!"
Kilipepesa macho mara kadhaa. "Ndiyo ninacho jaribu kufanya."
"Namaanisha huwezi kufanya hivyo!"
"Kwa nini?"
"Naam, hakuna mtu mwingine ameweza kuponya macho yangu, isipokuwa na miwani."
"Nina uwezo fulani. Utaona, ikiwa..."
"...sitamwambia mtu yeyote kuhusu wewe?"
"Ndiyo msingi wake, ndio kiini."
"Nitajuaje hutanipofusha? Unaweza kuwa kama wale wachuuzi ambao hutoa ahadi lakini wanadanganya kabisa."
Kilianza kupaka nta, kisha kuifuta tena. "Siwezifanya kitu kama hicho kwa kiumbe ambacho hakijanidhuru."
"Inamaanishaa kama ningekukuumiza, unaweza kunifanya kipofu?"
"Hiyo ni kwa msingi wa haja ya kujua."
"Na ikiwa utaponya macho yangu, na sitamwambia mtu yeyote kuhusu wewe, utaondoka mashambani mwetu?"
"Ndiyo msingi wake!" [...]